Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa serikali yake inajitahidi katika kuboresha hali ya uzalishaji wa bidhaa nchini Tanzania, lakini bado kuna hitaji la wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania katika kuboresha huduma na bidhaa zinazopatikana nchini humo na kuziuza kama bidhaa zilizo tayari kwa matumizi badala ya bidhaa-ghafi. Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa jumatano wiki hii wakati akiwahutubia watu waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi hati kwa mabalozi wa heshima wa Tanzania kutoka majimbo mbalimbali ya nchini Marekani, sherehe zilizofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini Washington DC
Sikiliza ripoti hii ambayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30am). Hii ilikuwa ripoti ya Septemba 21, 2013
|
0 Comments