Stori: Waandishi Wetu
JUZI jijini Dar es Salaam zilisambaa taarifa kuwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ amefutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kufuatia taarifa hizo, Risasi Jumamosi lilianza kuwatafuta watu wenye uhakika wa madai hayo ili kuujua ukweli. Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye orodha ya kutafutwa ni pamoja na Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, mchumba wa Masogange aliyepo Bongo, Evans Komu na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Afande Godfrey Nzowa.

ALIVYOSEMA AFANDE NZOWA
Wa kwanza kupatikana alikuwa Kamanda Nzowa ambaye  alisema:
“Ninachojua mimi, Agnes na mwenzake (Melisa Edward) bado wanashikiliwa. Kesi yao ilikuwa Jumatano (Septemba 18, 2013), itatajwa tena Novemba mwaka huu.”
Nzowa akapiga hatua zaidi kwa kusema kwamba aliwahi kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwahoji akina Masogange kabla ya kupandishwa kizimbani Jumatano iliyopita lakini hawakumpa ushirikiano.

BALOZI WA TANZANIA, AFRIKA KUSINI
Baada ya Kamanda Nzowa, Risasi Jumamosi lilimtafuta Balozi wa Tanzania Sauzi, Msuya akasema:
“Mimi sina uhakika, ilimradi umeniambia nitafanya hivyo maana nimekuwa nikifuatilia sana maisha yao wakiwa jela. Lakini pia napenda muwaambie vijana wa Tanzania, wanapokuja huku wawe kamili, waje kwa uhalali, wawe na fedha za kujikimu wakiwa huku mpaka watakaporudi.”

MCHUMBA WA MASOGANGE SASA
Baada ya kuzungumza na balozi huyo, Risasi Jumamosi lilimtafuta Evans na kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alikiri Masogange kuwa huru, akasema:
“Ni kweli mchumba ‘angu Agnes yuko huru. Wasiomjua ndiyo walikuwa wanasema, wameniambia mambo mengi sana kuhusu yeye lakini nilivumilia. Namshukuru Mungu Agnes amerudi tena mikononi mwangu.”
Evans alikwenda mbele zaidi kwa kumuunganisha mwandishi wetu na Agnes kule Sauzi ambapo walizungumza kwa dakika ishirini na mbili.
Risasi: Mambo Eg?
Masogange: Poa, mzima wewe?
Risasi: Mi mzima bwana, pole, nasikia uko huru?
Masogange: Ee, namshukuru sana Mungu.
Risasi: Hivi hebu niambie kwa ufupi, hali ya magereza ya huko ikoje?
Masogange:  Ni balaa, nimekuwa nikiishi maisha magumu sana. Unajua kuishi na watu ambao si taifa lako ni tatizo kubwa, hakuna amani, inachosha akili na kila kitu.
“Ilifika mahali nilitamani ningepata matatizo haya nikiwa nyumbani lakini si ugenini.”

AFUNGA NA KUOMBA
Agnes alienda mbele zaidi kwa kusema amekuwa akifunga na kuomba kila siku kwa muda wote akimlilia Mungu amsaidie kutoka kwenye janga lake.
“Nilifunga sana, pia nilikuwa naomba maombi mazito kabisa. Nimekonda kwa sababu ya kufunga huko.”

USAGAJI
Kuhusu vitendo vya usagaji, staa huyo alisema kuwa askari wa Sauzi wako makini sana na hilo na wanatoa somo kila mara linalokataza tabia ya usagaji na kwamba mtu akibainika anaweza kufunguliwa shitaka jipya.

ALIWAHI KUTILIWA SHAKA
Alisema alishawahi kuitwa na Melisa na kuulizwa kuhusu uhusiano wao, akajieleza kuwa ni mama mkubwa kwa mdogo, ikawa nafuu yao lakini walihisiwa vibaya kutokana na ukaribu wao.

ADAI ALIWAHI KUTONGOZWA NA ASKARI
Risasi: Tuliwahi kusikia kwamba kuna askari wanakutongoza kutokana na wowowo lako. Je, madai haya ni ya kweli?
Agnes: (kicheko), watu wanachonga sana. Unajua mimi nina mchumba wangu jamani.
Risasi: Lakini kuna ukweli wa madai hayo?
Agnes: (akakata simu).
Swali hapa linaweza kuwa hivi, kama hajaachiwa huru kwa nini aliongea na simu akiwa gerezani? Jibu lipo. Masogange amekuwa akipatikana hewani mara kadhaa licha ya kuwa gerezani.

WATU WAMSOMA KWENYE INSTAGRAM
Kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambao hakuwa hewani tangu Julai mwaka huu, usiku wa Septemba 17, 2013 aliandika hivi:
“Thanks God nimeamini wewe ulikuwa pamoja na mimi katika maombi yangu na thanks kwa wote mliokuwa mkiniombea, Mungu kapokea maombi yenu.”
Halafu akaendelea: All praise and glory to the Lord almighty I thank you for my freedom, amen (Sifa zote ni kwa Bwana, nakushukuru kwa uhuru wangu, amen).

LINAVYOSEMA RISASI JUMAMOSI
Risasi Jumamosi linaweka wazi kwamba, Agnes awe ameachiwa au hajaachiwa, lakini watu wote waliotafutwa ili wazungumze walipatikana na walisema kama ambavyo imeandikwa.

VIPI KUHUSU REHEMA FABIAN?
Wakati tunakwenda mitamboni kuna habari zilisambaa kwamba, Miss Kiswahili 2009, Rehema Fabian anadaiwa kukamatwa nchini China.
Madai yamesema mengi, lakini hakuna mwenye kusema wazi kisa nini ingawa wengine walidokeza habari za unga.