Jana katika uzinduzi wa filamu mpya ya kiswahili inayojulikana kwa jina la Our Special Family kulikuwa na matukio mengi sana ukumbini hapo,mojawapo ni la upigaji wa picha na mahojiano na wasanii wote walioshiriki katika filamu hiyo.Pichani ni ndugu Hija na mkewe Halima ambao pia walishiriki katika filamu hiyo,Hija ndiye mtunzi,muandishi na Director wa movie hiyo. 
 Moja ya vijana wakali wanaoibukia kwenye tasnia hii ya movie za kiswahili,kushoto ni Omar Abbas na Nico Gabino wakiramba Flash hapo jana
 Kutoka kushoto ni Naima,Halima na Sonia au Sexy Mama ambao pia kila mmoja alionyesha uwezo wa juu katika uigizaji
Waaawwwoooohhhh.....!!!
 Wadau ambao walihudhiria katika uzinduzi wa filamu hiyo hapo jana

 Madada warembo na watoto warembo
Maganga One Blog ilikuwa live katika urushaji wa kila kinachojiri ukumbini hapo,pichani ni msanii na mke wa Director shemeji langu la ukweli Halima akichapwa maswali 
 Mrembo Sakina ambaye ni mmoja kati ya washiriki wa movie hiyo pia nae alitandikwa maswali na Maganga One
 Bidada Naima mshiriki wa movie hiyo nae pia alikula maswali kutoka kwa Maganga One
Director wa movie akitoa utambulisho special kwa Bidada Rabia kwamba yeye ndiye aliweza kuwapendezesha washiriki wote walioshiriki movie hiyo kwa kuwaremba na nakshinashki ambazo zilikuwa bab kubwa,pembeni mwa Rabia ni star mdogo anayekuja kwa kasi ya ajabu ni Said Biboze ama Dj Biboze.