Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Dk. Asha-Rose Migiro atembelea Ubalozi wa Tanzania hapa London, kwa lengo la kuwasabahi maafisa wa Ubalozi na kuwapatia taarifa mbalimbali za maendeleo ya ushiirikiano na vyama marafiki na CCM, hususan Chama cha Labour cha Uingereza.
Mhe. Dk. Migiro alipita Ubalozini akitokea mji wa Brighton, Kusini mwa Uingereza alikokuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa wa Chama cha Labour uliofanyika huko kuanzia tarehe 22 hadi 25 Septemba 2013. Katika mazungumzo yake na maafisa hao Dk. Migiro aliwadokeza kuwa akiwa Brighton alifanikiwa kukutana na kuanzisha mawasiliano na maafisa mbalimbali wa Chama cha Labour kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano wa vyama vyao. 
Mheshimiwa Dk. Migiro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Amos Msanjila, Allen Kuzilwa, Rose Henry Kiondo, Wema Kibona, Idris Zahran, Caroline Kitana Chipeta na Yusuf Kashangwa.