Napenda kusema machache kuhusiana na ushindi mkubwa wa bondia Francis Cheka dhidi ya bondia kutoka Marekani.
Heshima aliyojijengea Cheka na Taifa kwa ujumla ni muhimu kwa upande wangu kumpongeza.Nina kila sababu ya kumpongeza kwa jitihada alizozionyesha mpaka kuupata ushindi huo.Kwanza la muhimu ambalo Cheka anastahili pongezi ni kuuchezea uwanja wa nyumbani vyema,amepewa chance kuwa sana kupambanishwa na bondia mzuri toka Marekani na hakufanya makosa kaitumia vyema nafasi hiyo.

Cheka hongeza sana hukutaka kuwatia aibu watanzania wenzako na hilo ndilo la msingi,kwa sasa una jina kubwa sana duniani na umeitangaza vyema nchi yako.Jitahidi kuulinda vyema mkanda wako kwani wamarekani katu hawakubali taji kubwa kama hilo alishikilie mwafrika,hivyo jiandae kupewa mapambano makubwa makubwa ili mradi tu wakuvue mkanda huo,ushauri wangu ni kuongeza mazoezi na usilewe sifa.Binafsi umenifurahisha sana na nakupongeza sana tena sana.