Stori: Imelda Mtema
SURA ya mauzo kwenye sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amesababisha usumbufu mkubwa kwa waalikwa wa bethidei ya chipukizi wa filamu, Mumy Mushi.Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Pub ya MV Gliterat, Kinondoni-Studio, jijini Dar ambapo Wolper aliyekuwa mgeni rasmi hakufika katika muda muafaka hivyo bethidei kushindwa kuanza hadi saa sita usiku.
“Tumechoka sisi kumsubiri huyo Wolper basi ngoja sisi tuondoke haiwezekani kila wakati anasema yupo karibu, kama hiyo keki utakula mwenyewe na huyo Wolper wako,” alisikika mualikwa mmoja ambaye hakutaja jina lake.
Hata hivyo, Wolper alifika kwenye sherehe hiyo saa 7 usiku wakati waalikwa wengi wakiwa wamekata tamaa na kutaka kuondoka.