Mhe. Balozi Liberata Mulaula katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei wakati wageni wakiingia kwenye hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza huduma mpya za kibenki kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite.( Picha na Vijimambo Blog)
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiingia kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulikofanyika hafla fupi iliyoandaliwa na CRDB Bank Jumatano Oct 9, 2013 kwa ajili ya kutambulisha huduma mpya za Benki hiyo kwa ajili ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwatamburisha waheshimiwa wageni kwa baadhi ya Watanzania walofika kusikiliza huduma mpya za Benki ya CRDB kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite na baadae kumkaribisha mkurugenzi mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei kuongea na WanDMV kwa niaba ya WanaDiaspora.
Waziri wa Fedha na Uchumi Dkt. William Mgimwa akiongea machache na kuwaambia wanaDMV wajisikie wapo Tanzania na salama kwani amekuja na ujumbe mzito unaowakilisha Bara na visiwani na baadae kumshukuru Mhe. Balozi Mulamula kwa makaribisho mazuri na CRDB Bank kwa kuandaa hafla hiyo fupi iliyofanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Jumatano Oct 9, 2013 jioni.
Waziri wa Fedha na Uchumi akiongoza ujumbe wake kwenye chakula cha jioni.
Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi Zanzaibar Mhe. Yussuf Mzee akibadilishana mawili matatu toka kushoto ni Mariam Mkama, Love Maganga na Tully Esther Mwambapa ambaye nia Director of Marketing, Reserch and Customer Service wa CRDB Bank.
0 Comments