MAHAKAMA yaHakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana imepiga kalenda kesi
inayowakabili watu 11 akiwemo Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Mohamed maarufu
kama Kisoki, dhidi ya mashtaka 24 ya
mauaji ya bila kukusudia yaliyotokana na gorofa 16 kuporomoka baada ya upande
wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mbali na
Kisoki washtakiwa wengine ni, Raza Ladha, Goodluck Mbanga, Willbroad Mugyabuso,
Ibrahim Mohamed au maarufu kama Kisoki, Mohamed Abdulkarim, Charles Ogare,
Zonazea Oushoudada, Vedasto Ruhale, Michael Hema, Albert Mnuo na Joseph Ringo.
Kesi hiyo
iliahirishwa na Hakimu Mkazi Devota Kisoka baada ya upande wa Jamhuri kudai
kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Wakili wa
Serikali Petronila Kisaka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika
na kwamba jalada la kesi hiyo liko kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi
Ilala (RCO).
Hakimu
Kisoka alisema kesi hiyo itatajwa tena Novemba 14, mwaka huu.

Katika kesi
hiyo, ilidaiwa kuwa Machi 29, mwaka huu
mtaa wa Indrira Gandh, Wilaya ya Ilala washtakiwa kwa pamoja waliwaua watu 20 bila
kukusudia.