Vijana nchini Afrika Kusini wakiadhimisha siku ya vijana duniani
Kile kinachosemekana kuwa mkutano mkubwa zaidi wa vijana unatarajiwa kuanza hivi punde mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Vijana efu moja miatatu kutoka katika mataifa ya 93, watahudhuria kongamano hilo liitwalo, dunia ya vijana katika uwanja rasmi wa michezo mjini humo.Watajadili maswala kama vile ajira kwa vijana, elimu na dhuluma za kingono.
Mkutano huu wa siku 4 utawajumuisha vijana 1300 chini ya umri wa miaka 30 kutokea mataifa 180 na mada kuu ni vijana kujifundisha utawala bora na kuwa viongozi wa kesho,ilimu ,haki za Binadamu, ukosefu wa ajira miongoni mwa mambo mangine mengi.Wengi ya vijana wanaume kwa wanawake wanaotarajiwa kuhudhuria kongamano hili ni vijana wanaotokea katika mataifa yaliokumbwa na misukosuko ya kivita lakini vijana wa vyama tawala kutoka serekali za mataifa hayo 180 hawakualikwa ilivyokua kongamano hili sio kongamano la kiserikali.
Baadhi ya vijana wanaotarajiwa kushiriki kwenye mkutano huu wa mara ya nne wa One Young World ni Kevin Musila na Billow Hassan kutokea Kenya , Arinitwe Stephen kutokea Uganda na Ilwad Elman kutokea Somalia.
Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, msanii wa muziki wa Rock, Bob Geldoff na mshindi wa tuzo ya Nobel kutoka Bangladesh Mohammad Yunis, ni miongoni mwa watakaowahutubia vijana hao
|
0 Comments