Al Liby alihusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za Kenya na
Tanzania mwaka 1998
Mwanamume raia wa Libya aliyekamatwa mapema mwezi huu katika
operesheni iliyofanywa na Marekani mjini Tripoli, amefikishwa nchini Marekani
kukabiliana na tuhuma dhidi yake.
Maafisa walisema kuwa Abu Anas al-Liby, ambaye jina lake halisi ni, Nazih
Abdul-Hamed al-Ruqai, alihojiwa akiwa kwenye meli ya kijeshi ya Marekani
kuelekea Marekani.
Anatuhumiwa kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya balozi za
Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998.
Bwana Liby alisemekana kuwa na makosa ya kujibu mwaka 2000 katika mahakama
moja mjini New York .
Mwendesha mashtaka mjini New York alisema kuwa Bwana Liby alihamishwa hadi
katika kituo cha sharia mwishoni mwa wiki jana.
Atafikishwa mahakamani Jumanne.
Marekani ilikuwa inamsaka sana Anas al-Liby na alipokamatwa kuhusiana na
operesheni iliyofanywa na wanajeshi wa Marekani tarehe 5 Oktoba, wengi waliona
operesheni hiyo kama iliyokiuka uhuru wa libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametetea hatua ya kukamatwa kwa
Libya, akisema kuwa alikamatwa kihalali.
Serikali ya Libya imeitaka Marekani kuelezea kuhusu kukamatwa kwa Libya kiasi
cha kumtaka balozi wa Marekani kufika mbele ya waziri wa sheria kufafanua kwa
nini Liby alikamatwa. |
0 Comments