Mkali huyo aliyekuwa nchini Marekani atapiga shoo Dar Live Jumatano ambayo ni Sikukuu ya Eid sambamba na Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Dimpoz amewataka mashabiki wake kutokosa shoo hiyo maana itakuwa ya aina yake. Ameeleza kuwa yeye pamoja na timu yake ya Poz kwa Poz watakuwa ndani ya nyumba kuwapa raha mashabiki. Katika sikukuu hiyo, Bendi ya Twanga Pepeta nayo itatoa burudani sambamba na Profesa Calabash atakayewapa burudani watoto.