Kipofu kampiga mtu mpaka kamuua, akafikishwa mahakamani;

HAKIMU: Kwanini umefanya ukatili namna hii

KIPOFU: Mheshimiwa marehemu alisema mwenyewe,'Ukinipiga utaona',

kwa vile nilikuwa na hamu kubwa ya kuweza kuona, nikajitahidi kumpiga sana ILI nipone, bahati mbaya kafariki.

HAKIMU: ushahidi haukutii hatiani, kwani kwa mujibu we mashahidi imedhihirika kuwa sababu ya mtuhumiwa kumpiga kwa bidii marehemu, ilichagizwa na maneno ya marehemu mwenyewe kuwa "mtuhumiwa akimpiga ataona" hivyo mahakama imejiridhisha kuwa mtuhumiwa aliua bila kukusudia, na inamuachia huru.

KIPOFU: Samahani Mh. Jaji, sasa pamoja na yote marehemu amekufa Kabla ya kuitekeleza Ahadi yake, mie bado sioni.