Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
WAANZA UHUSIANO KABLA YA NDOA Amos alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa baada ya kufikisha ombi hilo kwa baba yake, yeye na Mary wakaanza kuwa marafiki wa ‘baby’, ‘darling’, ‘sweet’ kama siyo laaziz achilia mbali mahabuba.
Anasema wakati huo Mary alikuwa na umri wa miaka 14 tu, lakini kwake hakuona kama ni sababu ya kutompata ili wawe wanapika na kupakua, yeye Amos alikuwa na umri wa miaka 16. Kwa hiyo walikaa mwaka mmoja katika uhusiano. Mh! Alisema wazazi wa Mary nao walipopelekewa ujumbe wa ushenga wakasema ‘asante Mungu’, wakawa tayari kumpokea Amos kuwa mume wa binti yao mpendwa, Mary.SIKU YA NDOA YAFIKA
Habari zilieleza kuwa siku ya ndoa hiyo ya kihistoria iliwasili, ndugu, jamaa na marafiki walifika nyumbani kwa mzee Sailowa kwa ajili ya kushuhudia Amos akipata jiko, akipata mke mwema na maandiko matakatifu yanasema mke mwema mtu hupewa na Bwana. Yeleuuwii! Baada ya ndoa kufungwa, sherehe za harusi ziliendelea nyumbani kwa akina Amos ambapo nyimbo ngoma na nyimbo za asili na kisasa ‘eti mlisema haolewi, mbona kaolewa’ zilitamba na kuifanya harusi hiyo itafsirike kuwa ya kihistoria kwa mwaka 2013 katika kijiji hicho.
WAALIKWA WALA, WANYWA Licha ya umri wa wanandoa kukosa vigezo vya kuoana, lakini waalikwa waliweza kula, kunywa na kuserebuka huku wakiwatakia maharusi maisha marefu yenye baraka, waje kupata watoto wa kike na kiume na wao waitwe baba na mama.
WASIMAMIZI NI WATOTO WENZAO! Katika hali ya kuendelea kushangaza zaidi ndoa hiyo ilisimamiwa wa watoto wenzao ambapo ‘matron’ ana miaka 15 na ‘patron’ miaka 16, ambaye naye ameoa huku msimamizi wa kike akisema ana mchumba, Mungu akijalia siku yoyote na yeye atafunga pingu za maisha kama si za milele.
DIWANI AZUNGUMZA Baada ya tukio hilo, paparazi alimtafuta diwani wa kata hiyo na kumuuliza kama analijua tukio hilo. “Mimi sikuwepo, nilikuwa kwenye majukumu mengine, lakini suala kama hilo linapotokea huwa linashughulikiwa. Huko nyuma yamewahi kutokea matukio kama hayo, wahusika walifungwa jela. “Hata hili, kwa sababu ndiyo unaniambia, nitalifuatilia, kama ni kweli wamefunga ndoa wakiwa katika umri wa chini ya miaka ya kisheria ya kumi na nane, watachukuliwa hatua wao na wote walioidhinisha,” alisema diwani huyo.
KAZI YA BWANA HARUSI Katika mazungumzo yake, Amos alisema kazi inayomfanya apate nguvu ya kuoa kwa mbwembwe ni ufundi seremala ambapo yeye ni stadi katika kazi hiyo.
ANACHOSEMA BI HARUSI Kwa upande wake bi harusi Mary aliweka bayana kwamba, hana kazi, ila akiwezeshwa anaweza kufanya biashara ya kuuza maandazi.
WAZIRI SOPHIA SIMBA UNALO HILO! Kwa mujibu wa watu nje ya kijiji hicho ambao walishangazwa na tukio hilo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ana kazi kubwa ya kufanya juu ya matukio kama hayo yaliyoshamiri katika jamii.
|
0 Comments