Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania London unawakaribisha Watanzania wote watakaoweza kupata fursa kuja kuzungumza na Waziri wa Sheria na Katiba, Mheshimiwa Mathias Chikawe na Wawakilishi kutoka
Wizara ya Sheria na Katiba - Tanzania, hapa Ubalozini siku ya Ijumaa (tarehe 01 Novemba 2013) kuanzia saa Tisa alasiri (15:00).
Mheshimiwa Waziri anatarajiwa kuzungumzia masuala mbalimbali ya Sheria na mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania unaondelea hivi sasa. Mhe. Waziri Chikawe anatarajiwa kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi watakaohudhuria mkutano huo. IMETOLEWA
NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA