Na Musa Mateja
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, ameendelea ‘kuhenyeshwa’ na misiba ya wakwe zake kufuatia mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’ kufiwa na baba yake mdogo, Boniface Mungilwa.Msiba wa marehemu huyo ulikuwa Magomeni jijini Dar na alizikwa Jumatatu iliyopita. Diamond alifika msibani hapo na kujumuika na waombolezaji wengine.
Hivi karibuni, Diamond alifiwa na ‘baba mkwe’ wake mwingine, mzee Isaac Abraham Sepetu ambaye ni baba mzazi wa mpenzi wake, Wema Sepetu mazishi yalifanyika Zanzibar ambapo pia Diamond alihudhuria.