Miss Universe Tanzania 2013, Betty Omara.
Mashindano ya 62 ya urembo ya Miss Universe yanatarajiwa kufanyika leo usiku  katika Ukumbi wa Crocus City, Krasnogorsk, Moscow nchini Urusi . Olivia Culpo, Miss Universe 2012 kutoka Marekani atamvisha taji mrithi wake atakayeshinda katika shindano hilo litakalowashindanisha warembo kutoka nchi 86. Mwaka huu, Tanzania inawakilishwa na mrembo Betty Omara.