Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwana wa Malkia  Elizabeth II wa Uingereza, Prince Charles,  jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 15, 2013 pembeni ya mkutano wa Wakuu wa nchi za Junuiya ya Madola (CHOGM 2013) ambako Prince Charles, maarufu zaidi kama His Royal Highness the Prince of Wales, anamwakilisha mama yake mwenye umri wa miaka 87 ambaye hakuhudhuria kwa mara ya kwanza katika miaka 40 ya historia ya mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi itayoteuliwa mwishoni mwa mkutano. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe Peter Kallaghe.

Malkia Elizabeth wa II alihudhuria CHOGM kwa mara ya kwanza mwaka 1973 jijini Ottawa, akiwa kakosa kikao cha mwaka 1971, na tokea hapo hajakosekana tena hadi safari hii. Alikuwepo pia katika mkutano wa mwisho uliofanyika mwaka 2011 jijini  Perth, Australia. Na hii ni mara ya kwanza kwa Prince Charles kumwakilisha mama yake ambaye imesemekana hakwenda Sri Lanka kutokana na ushauri wa kutosafiri umbali mrefu. Ila katika CHOGM 2007 iliyofanyika Kampala, Uganda, yeye na mama yake walihudhuria pamoja.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kikao cha ufunguzi cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola jijini Colombo Srilanka leo asubuhi.kushoto ni Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague