Stori: Na Hamida Hassan
IKIWA anakaribia kufikisha mwaka mmoja tangu afariki dunia, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, dua maalumu ya kumbukumbu inatarajiwa kusomwa Novemba 26, mwaka huu.
Akizungumza na Chanzo cha habari hizi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, mchekeshaji wa kike, Sherry Magali, alisema ameandaa dua itakayosomwa nyumbani kwake Mabibo, Dar siku hiyo kwa sababu pia ni siku yake ya kuzaliwa.
“Mimi na Sharo tunashea siku ya kuzaliwa. Sharo amefariki siku yake ya kuzaliwa, kwangu mimi nimeona ni vyema kufanya dua hii muhimu kwa lengo la kumkumbuka mwenzetu,” alisema Sherry.