Brandts ambaye yupo katika kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho. 
…………………………………………………………………………..
KOCHA Mkuu wa Yanga Ernie Brandts, amegoma kuendelea na kazi kama alivyokubaliana na uongozi huku akisisitiza kwamba ana kikao na uongozi kuweka sawa baadhi ya mambo.
Brandts ambaye yupo katika kuitumikia notisi ya siku 30 aliyopewa na uongozi wa Yanga ikiwa ni mpango wa kumuondoa katika cheo chake hicho, alishindwa kuibuka katika mazoezi ya kikosi hicho, yaliyoendelea jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama, Dar es Salaam akimuachia msaidizi wake, Fred  Minziro.
Habari ambazo Mwanaspoti, imezipata baada ya Brandts kutoonekana katika mazoezi hayo, zinadai kwamba kocha huyo alishindwa kutekeleza kwa vitendo kuendelea kukifundisha kikosi hicho, badala yake amekuwa akitaka kukutana na mabosi wa timu hiyo, kujadiliana nao jambo moja muhimu.
Imeelezwa kuwa Brandts, ameona hataweza kuendelea kukifundisha kikosi hicho, baada ya kubaini kuwa kuendelea kukifundisha kikosi hicho ndani a siku 30, hakutakuwa na maana tena kutokana na tayari viongozi wa Yanga, wameonyesha nia ya kumuondoa huku wakianza taratibu mchakato wa kumsaka mrithi wake, ikiwa ni kufikia mwisho kwa utawala wa Mholanzi huyo aliyedumu kwa msimu mmoja na nusu.
Habari zinasema Brandts alipanga kukutana na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga jana jioni kumalizana naye ili asiendelee na majukumu yake kwa vile ameona hayatakuwa na tija katika kikosi hicho.
Brandts alipoulizwa alisema: “Nimeshindwa kuja mazoezini, hicho ndicho ninachoweza kukwambia kwa sasa, sitaki kuongea nawe kwa kirefu naomba uelewe hilo, nasubiri leo(jana) jioni naweza kukutana na uongozi kuna jambo nataka kujadiliana nao.”
CHANZO: MWANASPOTI