Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo
jipya la Kiwanda cha Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali, huko Maruhubi Mjini Unguja,ikiwa ni katika shamra shamra za
Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa
Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)
alipotembelea jengo jipya la kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa
ni shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh
Rajab,kuhusu mashine mpya zilizonunuliwa na idara ya uchapaji,wakati
alipotembelea kuangalia mashine kuona utendaji wake kazi,baada ya
kufanya unguzi rasmi,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi
ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akiuliza suala kwa Mkurugenzi Kanda wa
Kampuni ya MFI DOCUMENT SOLUTION LTD, Rama Subramanian,ikiwa ndio
wataalam wa mshine za uchapishaji,alipotembela na kuona
zinavyofanyakazi,wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda
hicho,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa
mashine ya CTP,ambayo inatoa picha kwa kutumia Plat,Mohamed Abass
Rajab,(wa tatu kushoto) wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda
cha Uchapaji cha Zanzibar jana,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]