Majaji wa shindano la epiq bongo star search 2013,  wakifuatilia shindano hilo lililofanyika jana Club 
ya Escape, Mikocheni Dar es Salaam ambapo  Emanuel Msuya kutoka jijini Mwanza aliibuka
 mshindi na nafasi ya pili kuchukuliwa na Elizabeth  Mwakijambile. Kutoka kushoto ni Banana Zoro, Jaji 
Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bench Mark  Production waandaaji wa shindalo hilo, Ritta   Pausen na Joackim Kimaro ‘Master J’. 
Mshindi namba mbili Elizabeth Mwakijambile, akishambulia jukwaa wakati wa shindano hilo.

 Washiriki watano wa shindano hilo wakisubiri kuchujwa  wawili kati yao. Kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emanuel Msuya,Melisa John, Maina Thadei na Amina Chibaba.
 Washiriki walioingia tatu bora wakisubiri mmoja wao  kuondolewa. Kutoka kushoto ni Elizabeth Mwakijambile,  Emanuel Msuya na Melisa John.
Emanuel Msuya na Melisa John akiwa chini huku akishangilia ushindi wake. 
Mkurugenzi wa Bench Mark  Production waandaaji wa shindalo hilo, Ritta   Pausen akikumbatiana na mshindi wa shindano hilo Emanuel Msuya. 
 Mshindi wa Shindano la epiq bongo star search 2013 Emanuel Msuya (katikati), akiwa amebeba sanduku   lenye kitita cha sh. milioni 50 alichokabidhiwa naMkurugenzi wa Bench MarkProduction Ritta Poulsen   (kushoto), baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo,   Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha   Fedha wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Ali Bakari ambayo imetoa fedha hizo na wadhamini wakuu wa shindano hilo.
Mashabiki mbalimbali walioudhuria katika shindano hilo.