Bunge la Somalia limeanza kujadili hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon ambaye amekuwa haelewani na rais wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mahamud.
Bwana Shirdon hivi karibuni amekuwa akimkosoa rais wa nchi hiyo kwamba amekuwa akiongoza nchini hiyo bila kufuata katiba.
Wafuasi wa rais Hassan wanasema Waziri Mkuu huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake na uongozi wake umekuwa hauna mafanikio.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo Somalia anasema mgawanyiko katika serikali ya Somalia iliyoundwa mwaka jana, unatishia juhudi za kuimarisha utulivu nchini humo baada ya nchi hiyo kuathirika na mgogoro kwa takrabani miongo miwili.
0 Comments