Mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick (akiwa amefunikwa uso) mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi 66 za heroin tumboni. 
 Polisi wakichunguza pipi zenye dawa za kulevya alizokutwa nazo mrembo anayedaiwa kuwa Jack Patrick.
Wanahabari nchini China wakichukua picha za dawa hizo za kulevya anazodaiwa kukutwa nazo Jack.
MODO maarufu Bongo, Jacqueline Patrick Cliff, anadaiwa kukamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao nchini China. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya pipi 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720 sawa na shilingi milioni 215.5 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Jack alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne ya Desemba 19, 2013. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko China.