Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu David Pelo Kivuyo aliyekuwa Diwani wa zamani wa Makuyuni. Marehemu Pelo, ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, alifariki tarehe 22 Desemba mwaka huu na kuzikwa nyumbani kwake Makuyuni jana Desemba 28. Alifariki kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.