Mkalimani ambaye alikuwa akitazamwa na watazamaji duniani kote katika kumbukumbu za maombolezo ya aliyekuwa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini hayati Nelson Mandela inasemekana alikuwa ni  bandia {Fake Translator}.Kwa mujibu wa wa shirikisho la watu viziwi nchini Afrika Kusini{ South Africa's deaf federation}. waliokuwa wakifuatilia hotuba ya Rais wa Marekani bwana Barack Obama wamelalamika kwa kutomuelewa mkalimani huyo.

Mkurugenzi wa shirikisho la watu wasiosikia bwana Bruno Druchen alieleza masikitiko yake baada ya kusikia malalamiko toka kwa walemavu wa watu wasiosikia kulalamika kwa kile kinachodaiwa kutomuelewa mkalimani kwa kile alichokuwa akikitafsiri,wataalamu wa mambo ya kutafsiri wanaelezea kwamba ni ukweli husiopingika kuona yule mkalimani akiyumbisha mikono yake tofauti na maneno yanayoelezwa na rais wa Marekani.

Madai hayo ya aibu ambayo yamewakasilisha wananchi wa Afrika ya kusini waliokuwa wakiangalia hotuba mbalimbali za baadhi ya viongozi na Rais wa nchi hiyo bwana Jacob Zuma yalitokea jana katika kiwanja kikubwa cha mpira kijulikanacho kama FNB stadium.