Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt.Christina Ishengoma amewapongeza wananchi wa mkoa huo kwa ushirikiano wao katika shughuli za kujiletea  maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dkt.Christina Ishengoma amesema katika kipindi cha mwaka 2013 wananchi wa mkoa wa Iringa wamekuwa wakifanyakazi kwa kujituma na kwa ushirikiano mkubwa.
Kwa upande mwingine  ishengoma amewataka wananchi wote wa mkoa wa iringa  kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa sasa  kupanda mazao yanayovumilia ukame ambayo ni Mtama, Muhogo, Viazi vitamu na Ulezi kwa na kila familia ihakikishe inapanda chini ya hekari mbili.
Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutawahakikishia uhakika wa chakula hasa maeneo ambayo hupata mvua chache. Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo amewaasa wananchi kutumia mbegu bora za kilimo,mbolea ya kundia na kukuzia hasa kwa mazao ya mahindi na mpunga ili kupata mazao bora.
 
Aidha Ishengoma amewatakia heri ya krismasi na mwaka mpya huku akiwahakikishia kuimalishwa kwa ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu.