Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki.
RAIS Jakaya Kikwete amekubali kuwavua vyeo vyao Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk David Mathayo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki aliyekuwa tayari ametangaza bungeni kujiuzulu. Taarifa hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, bungeni baada ya kueleza kuwa ameongea na Rais na kukubali kuwavua nyadhifa zao kutokana na ripoti ya Operesheni Tokomeza iliyosomwa  bungeni jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli.

                                                                  Source