Huku Umoja wa Mataifa ukijiandaa kutuma maelfu ya wanajeshi zaidi wa kutunza amani Sudan Kusini, viongozi wa jamii ya kimataifa wanaendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano yanayoendelea nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ametoa wito kwa rais wa Sudan Kusini, Salva Kirr, na aliyekuwa makamo wake, Salva Kirr, kuanzisha mazungumzo ya amani.Uchina pia imetoa wito kuwa mapigano yasitishwe.
Kuna taarifa kwamba kumetokea mapambano Malakal, mji mkuu wa jimbo la mafuta la Upper Nile state.
Wanajeshi wa serikali wanasema wameukomboa mji muhimu wa Bor.
Mwandishi wa BBC anasema haikuelekea kuwa ghasia zitamalizika karibuni - ghasia zilizozidisha uhasama wa kikabila na kupelekea maelfu kuhama makwao.
0 Comments