Bwawa la kuogelea 'swimming pool' likiendelea kujengwa kwenye mjengo wa Diamond, Tegeta, Dar.
Staa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' anajenga bwawa la kuogelea 'swimming pool' katika nyumba yake anayoendelea kujenga huko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, staa huyo ametupia picha ya swimming pool hiyo inayoendelea kujengwa na kuandika yafuatayo: "Wachina wa nini wakati Watanzania wenzangu wanaweza pia???... #SwimmingPool #MyNewHome! Can't wait"