Stori: Mwandishi Wetu KUNA mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali wa kiroho, moja wapo ni hili la kuanzishwa kanisa la wala nyasi nchini. |
Gazeti hili lilifika Upanga, kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ndilo kanisa hilo lakini hakuna mtu aliyekutwa hapo.
Hata hivyo, baadhi ya majirani walisema huwa wanawaona watu wakiingia katika nyumba hiyo lakini ajabu kunakuwa hakuna kelele zozote.
Chanzo chetu cha habari kimesema kuwa waumini wa kanisa hilo hula nyasi na baadaye kutapika, hali inayowafanya waamini kuwa kwa kufanya hivyo, wametakasika kiroho kwa kujazwa Roho Mtakatifu.“Mchungaji wao huwakusanya waumini wake wanaopandisha mashetani wakiwa kanisani, hiyo hufanya shetani kumtoka mtu haraka,” kilisema chanzo.
Habari zinasema huduma hiyo ilianzishwa Afrika Kusini na Mchungaji na Nabii Daniel Lesego mwaka 2002.
Imedaiwa kuwa kwa sasa waumini hao wapo kwenye mfungo ambao watu hufika kanisani na baadaye kula majani yaliyopo nje ya kanisa hilo wakisema kwamba Roho Mtakatifu huongoza mtu kula chochote huku ikidaiwa kuwa manyasi hayo ni chakula kutoka mbinguni.
Gazeti hili linaendele kufuatilia habari hii.
Gazeti hili linaendele kufuatilia habari hii.
0 Comments