Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.
“Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”
|
0 Comments