Shukurani kwa Watanzania waishio DMV na State nyingine
hapa Marekani kwa kufanikisha kumsafirisha kwa mazishi ya mpendwa wetu Zaynab
Haroun Buzohera ( Zay B, Zay Dulllah).
Mimi  Ngalu Mariam Buzohera, Yusuf Buzohera wadogo
wa marehemu, mumewe Dullah, kamati ya mazishi Rais wa jumuiya ya watanzania
DMV,IddI Sandaly, Said Mwamende ,Jabir Jongo ,Hidaya Mahita,
Catherine Mukami, Irene Milembe na Latifa Mzese. tunapenda kuchukua nafasi hii
kuwashukuru watanzania wote mnaoishi hapa DMV,  Texas, New York, New
Jersey, Massachusetts, Ohio, California,North Calorina, Illinois na state
nyingine zote kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidiana nasi kufanikisha shughuli
nzima ya matayarisho na hatimaye kuwezesha kumsafirisha mpendwa wetu
kwenda kupumzishwa nyumbani Tanzania na mliweza kuwa nasi kuanzia hospitalini,
msibani na kutufariji nyumbani kwa marehemu na hadi sasa.
Tunapenda  kuwashukuru sana watu wa media zikiwemo
blogu ambazo zilitusaidia kutangaza habari za msiba, zikiwemo vijimambo,
Swahili villa, Swahili blog, Michuzi, Sunday Shomary, Je huu ni uungwana Blog,
Changamoto yetu, Jestina George Blog, Lukaza Blog, Sufiani Mafoto Blog,Mtaa kwa
mtaa Blog na nyinginezo na watu mbalimbali waliosambaza habari hizi za msiba
kwa njia ya text za aina zote, simu, facebook, instagram na vihabarishi
mbalimbali bila kumsahau Dada yetu wa DMV Tuma Katule kwa jinsi alivyoendesha
harambee.
Tunapenda kutoa shukurani za pekee wa Watanzania
wenzatu waliowahiishi DMV na wanaoendelea kuishi ambao walituwakilisha wenzao
wa Marekani kwa kujumika na familia ya mpendwa wetu nyumbani Tanzania tangia
siku ya kwanza ulipotokea msiba huu mpaka siku ya mazishi.
Shukurani zetu za dhati kwa aliyekuwa Balozi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar na
mumewe Shariff Maajar wakiwemo aliyekuwa Mwambata wa Jeshi kwenye Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga na mkewe Love
Maganga kwa ushiriki wao wa kuwafariji wafiwa nyumbani Tanzania tangia siku
waliposikia msiba huu.
Shukurani za pekee kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwa kujumuika na wafiwa
nyumbani kwao Ukonga Banana pia tunapenda kuwashukuru maafisa wa ubalozi wa
Tanzania hapa Marekani kwa ushirikiano wao wa hali na mali waliouonyesha.
Tunapenda kutoa shukurani kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Bara na Mbunge wa Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba kwa kutafuta muda wake na kuweza
kufika nyumbani kwa wafiwa Ukonga na kujumuika nao.
Kama kuna yeyote tutakuwa tumemsahau kwa njia moja au
nyingine tunaomba utuelewe sio kusudio letu kufanya hivyo tunathamini mchango
wako wa hali na mali uliosaidia na hatimaye kuwezesha na kufanikisha mazishi ya
mapendwa wetu.
Hatuna tutakacho walipa kitakacholingana na yote
mliotufanyia zaidi ya kumuomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awalipe.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu ampumzishe mpendwa wetu
Zainab Buzohera mahali pema peponi na sisi wote tuzidi kuombeana Kheri.


Innah Lillah wa Inaillah Rajiun ( Sisi ni wa Mola na
kwake tutarejea).