Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo (aliesimama) akitoa ripoti fupi mbele
ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati
na Madini juu ya miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini
walipomtembelea ofisini kwake ili kuelezea nia yao ya kufanya ziara katika
mkoa huo.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini
wameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
wizara hiyo kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika mikoa ya kanda
ya ziwa.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Victor Mwambalaswa,
kamati hiyo ilipata nafasi ya kupokea taarifa fupi kuhusu utekelezwaji wa
miradi hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist
Ndikilo ambaye aliwaeleza namna sekta hiyo inavyochangia katika kuinua
vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa kuhusu mahitaji ya umeme Mkoani humo alieleza kuwa kiasi
cha juu kinachotumiwa na mkoa huo ni megawati 46 na kuongeza kuwa ,
kiasi hicho kinaonesha mahitaji halisi na umuhimu wa nishati hiyo na
namna umeme unavyochangia ukuaji wa uchumi mkoani humo.
Akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu ya umeme, alieleza
kuwa ujenzi huo umeshika kasi na kuongeza kuwa tayari tayari mradi
uliotekelezwa na Millenium Challenge Corporation (MCC) umekamilika
wakati miradi mingine inayotekelezwa na REA na Electricity Five
inaendelea ambapo takribani wilaya 9 za mkoa wa mwanza zimeguswa na
miradi hiyo. Aidha alisema mradi wa REA phase 1 unajegwa na mkandarasi toka
Symbion umegusa wilaya ya Sengerema, Magu na Ukerewe, REA awamu
ya pili utaigusa wilaya za Magu, Misugwi, Ukerewe, Sengerema na kwimba
na kumalizia kwa mradi wa electricity five unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo Afrika kuwa unagusa wilaya za Magu, Misubwi, Kwimba,
na Sengerema ambapo alisema katika mradi huo ulipwaji wa fidia kwa
wananchi watakaoathirika umeshaanza. ‘‘Kazi ya usambazaji wa umeme Mkoani Mwanza inakwenda vizuri,
kukamilika kwa miradi hii kutasaidia vijiji vingi kuwasha umeme hivyo
kukuza pato la taifa’’ alisema Ndikilo. Alimalizia kwa kuwataka wajumbe hao kuwafahamisha wananchi kutumia
vipato na akiba zao katika kujenga nyumba zenye ubora ili waweze
kuunganishwa na huduma ya umeme. Vilevile Mhe Ndikilo aliwaomba wajumbe kuwaeleza wananchi
wanaowahudumia kujenga mazoea ya kuwa na mwamko wa kupokea na
kupenda maendeleo yanayopelekwa kwao na serikali. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati jhiyo Mhe. Victor Mwambalaswa
akipokea taarifa hiyo alieleza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa idadi
ya watu waliounganishiwa umeme inapanda toka asilimia 14 hadi kufikia
asilimia 30 ifikapo 2015. |
0 Comments