Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka
Dar es Salaam.
Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amekamilisha uteuzi wa majina ya Wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, litakaloanza vikao vyake Februari 18 mjini Dodoma.
Kupitia uteuzi huo amewarejesha bungeni wanasiasa wakongwe akiwamo Kingunge Ngombale Mwiru na Paul Kimiti na kuwakumbuka pia wanasiasa wakongwe ambao hawakuwahi kuwa wabunge.
Baadhi ya wanasiasa hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha (NLD) Dk Emmanuel Makaidi na Mwenyekiti wa Chama cha Ustawi Tanzania(Chausta) James Mapalala.
Pia wamo Mwenyekiti wa Chama chaDemocratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na John Chipaka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tadea.
Bunge hilo litajumuisha wabunge wote 357 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wajumbe 82 wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na 201 waliotangazwa jana na kufanya idadi yao kuwa 640.
Akitaja majina hayo jana Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka alisema wajumbe hao wameteuliwa kutoka katika makundi 10 ya kijamii.
Aliyataja makundi hayo na idadi ya walioteuliwa katika mabano kuwa ni Taasisi zisizo za Kiserikali (20), Taasisi za Dini (20), Vyama vya Siasa (42), Taasisi za Elimu (20), Makundi ya Walemavu (20), Vyama vya Wafanyakazi (19), Vyama vya Wafugaji (10), Vyama vya Wavuvi (10), Vyama vya Wakulima (20) na Makundi yenye Malengo yanayofanana (20).
“Taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao yaliyojumuisha majina 2,762 kwa upande wa Bara na upande wa Zanzibar yalihusisha watu 874,” alisema na kuongeza:
“Majina yote yalikuwa 3,636, lakini kinyume na sheria watu 118 walipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754. Taasisi hizo zilileta majina mengi na kazi ya kuyachuja mpaka kubaki 201 ilikuwa ngumu,” alisema Turuka.
Alisema uteuzi huo umezingatia umri wa waombaji na kwamba wenye umri kuanzia miaka 22 hadi 35 wapo 35, wenye umri wa miaka 36 hadi 60 ni 145 na kuanzia miaka 65 na kuendelea wapo 21.
“Wameteuliwa kwa kuangalia umri, jinsi, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika. Wanawake wapo 100 na wanaume wapo 101, wajumbe waliotokea Zanzibar ni 67 na waliotokea Tanzania Bara ni 134,” alisema.
Alisema katika kila kundi wajumbe kutoka Tanzania Bara wapo theluthi mbili na wale kutoka Zanzibar theluthi moja.Katika kundi la Taasisi zisizokuwa za Kiserikali watu maarufu walioteuliwa ni pamoja na Paul Kimiti, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Ajira na Maendeleo ya Vijana na Waziri wa Kilimo na Biashara, kati ya mwaka 1995 na mwaka 2000.
Mbali na Kimiti, pia yupo Kingunge, ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwamo uwaziri katika Serikali za awamu zote nne, tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa upande wa Taasisi za Kidini yupo ProfesaCosta Mahalu, Askofu wa Dayosisi ya Kati Kanisa la Mennonite, Amos Muhagachi, Sheikh Mussa Yusuf Kundecha na Sheikh Hamid Masoud Jongo.
Vyama vya Siasa yumo Shamsa Mwangunga ambaye amewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Majina kamili ya Wajumbe wa Bunge hilo ni :
2. Kingunge Ngombale Mwiru
6. Valerie N. Msoka
7. Fortunate Moses Kabeja
8. Sixtus Raphael Mapunda
10. Happiness Samson Sengi
1. Idrissa Kitwana Mustafa
4. Salama Aboud Talib
Taasisi za Dini- (Wajumbe20)
4. Mchungaji Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo
6. Askofu Donald Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora
9. Askofu Amos J. Muhagachi
13. Profesa Costa Ricky Mahalu
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
5. Louis Majaliwa
6. Yasmin Yusufali E. H alloo
Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu– (Wajumbe 42)
|
0 Comments