Kiongozi wa ujumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya mambo ya nje, Hamadi Yussuf Masauni (wa pili
kulia) akiwa na balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Begum Taj (wa tatu kushoto) na wajumbe wengine
wa kamati hiyo, John Shibuda (wa kwanza kushoto), Leticia Nyerere, Ibrahim Sanya na katibu wa
msafara huo, Rubi Laki. Picha na Mpigapicha Wetu. Mwandishi Wetu, Paris Ufaransa.
Kamati ya Bunge ya Masuala ya Mambo ya Nje imemaliza ziara ya siku
tatu nchini Ufaransa na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini
humo lililopo jijini Paris.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, kiongozi wa msafara huo Mhandisi Hamad Yussuf Masauni
alisema kamati imeridhishwa na utekelezaji wa mpango wa kununua jengo hilo kwa ajili ya matumizi ya
ofisi hivyo kuiepusha serikali na ghamara za ukodishaji.
Masauni alisema kupatikana kwa jengo hilo kutakuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi
na biashara baina ya Tanzania na nchi hiyo hususan kipindi hiki ambapo nchini inatekeleza itifaki ya
diplomasia ya uchumi.
Masauni ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kikwajuni (CCM), alibainisha kuwa diplomasia ya uchumi
imelenga kukuza uwekezaji na kuimarisha sekta ya utalii mpango ambao unatekelezwa katika nchi za
Ufaransa, Algeria, Morroco ba Ureno.
Alisema mazungumzo na wadau na taasisi mbalimbali nchini umo huenda yakafungua wigo mpana zaidi
katika sekta hizo mbili za uchumi ambazo ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya Taifa na kwa wananchi
wa pande zote mbili kwa ujumla wake.
“Ziara imekwenda vizuri na tumeweza kujifunza na pia kufungua mlango mwingine wa mashirikiano
baina ya Tanzania na baadhi ya wadau nchini humo” alisema na kuongeza kuwa kuna makapuni mengi
ambayo yana nia ya kuja kuwekeza nchini na katika sekta ya utalii.
Alisema jitiohada zaidi zinahitajika katka kuvitangaza vivutio vya utalii nchini ambavyo vingi bado
havifahamiki nje ya nchi ingawa serikali kupitia Wizara ya Maliasilio na Utalii inafanya jitihada
mbalimbali kutimiza azma hiyo.
Awali kabla ya kupatikana kwa jengo hilo, serikali ilikuwa inatumia wastani asilimia 34 ya bajeti nzima
ya ubalozi huo kwa aili ya kulipa pango kwa aili ya ofisi na nyumba za wafanyakazi wa ubalozi jambo
ambalo lilikuwa linaigharimu serikali na kuwazidisgia mzigo wa ugumu wa maisha wananchi wa kawaida. |
0 Comments