Libya imekamilisha uharibifu wa silaha za kemikali katika mpango ulioanza miaka tisa iliyopita chini ya uongozi wa aliyekuwa rais, Muammar Ghaddafi.
Tangazo hilo lilipitishwa katika mkutano wa wanahabari uliofanyika Jijini Tripoli na kuhudhuriwa na wajumbe wa kimataifa .Ikisaidiwa na Marekani, Ujerumani, na Canada, Libya imeharibu shehena ya sumu ya mvuke pamoja na silaha nyengine zenye sumu.
Katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Shirika la Silaha za kemikali zilizopigwa marufuku amepongeza Libya kwa kuchukua hatua hiyo muhimu.
Amesema kwamba hatua hiyo ni mfano mwema wa ushirikiano wa kimataifa ambao unaigwa na taifa la Syria kwa kiwango kikubwa.

Kwenye mkutano huo waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya ameeleza kwamba hatua hiyo ni ya kihistoria na ni mafanikio kutokana na ushirkiano na washirika wa kimataifa.
Mnamo mwaka wa 2004,Libya ilikuwa na takriban tani 13 za sumu ya mvuke.
Mrundiko huo wa kemikali hatari kwa sasa umeharibiwa.