TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya England baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Stoke City jana ikiwa ni mechi ya nane kupokea vipigo katika ligi hiyo.
Mabao yote ya Stoke yamefungwa na Charlie Adam katika dakika ya 38 na 52 wakati bao la Manchester United likifungwa na Robin van Persie dakika ya 47. Kwa matokeo ya jana, Man Utd imebaki na pointi zake 40.
Katika mechi ya jana, wachezaji wawili wa Man Utd, Jonny Evans na Phil Jones waliumia ambapo Jones alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kugongana na Jon Walters wa Stoke.
|
0 Comments