Mkuu wa kitengo cha mfuko wa huduma za jamii cha Vodacom "Vodacom Foundation"Yessaya Mwakifulefule (kushoto)akimsikiliza  Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni hiyo Suraya Hamdulay,wakati alipotembelea darasa la mafunzo ya kompyuta katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzaniakwa kushirikiana na Samsung.

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Lay Salumu akimuonesha Mkuu  wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay,jinsi wanavyojifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta mpakato wakati alipotembelea darasa hilo la mafunzo ya kompyuta katika Shule hiyo,kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.

Mwalimu wa somo la kingereza wa shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,Editha Mwinuka(wapili kutoka kushoto)akimwelekeza mwanafunzi wa kidato cha tatu Barnaba Siyame jinsi ya kupata matirio ya kujisomea katika kopyuta wakati Mkuu wa Biashara Endelevu wa kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kulia)alipotembelea Shule hiyo kujionea maendeleo ya mradi wa mpango wa kuziunganisha shule za Sekondari na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano,Uliofadhiliwa na Vodacom  Tanzania kwa kushirikiana na Samsung.kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Theresia Ng'wigulu.

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya sekondari ya Kambangwa jijini Dar es Salaam,wakijisomea .