Watu walioathirika na vita mjini Bangui |
Amesema wapiganaji hao ambao walikuwa watetezi wa jamii, wamegeuka na kuwa wauaji na waporaji.
Maelfu ya Waislamu wameukimbia mji huo na kukimbilia nchi jirani yaCameroon.
Hata hivyo ushahidi wa mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Seleka unaendelea kutolewa.
Misikiti yabomolewa
Mwandishi wa BBC, mjini Bangui, Kassim Kayira, anasema kuwa, Waislamu wengi wamepiga kambi katika msikiti mkubwa zaidi nchini humo, baada ya misikiti mingine kuharibiwa, huku Wakristu nao wakipiga kambi karibu na uwanja mkuu wa Ndege.Aidha amesema hali katika kambi hiyo ni ya kusikitisha huku wakimbizi hao wa ndani wakihitaji misaada ya dharura kama vile vyakula na dawa.
Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty internation limesema kinachotokea CAR ni kumalizwa kwa jamii.
Ripoti hiyo imetolewa wakati maelfu ya Waislamu wanendelea kuukimbia mji mkuu Bangui wakielekea nchi jirani.
Wakati huo huo Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema ndege ya kwanza iliyosheheni misaada imewasili katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati Bangui.
0 Comments