WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC jana
wamepokea kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa JKT Ruvu katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Nayo Azam FC waliokuwa wenyeji wa Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya bao 2-2 katika Uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar.