Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai, akiendesha Ibada bya Misa maalum ya Shukrani kufuatia kifo cha Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma (100), aliyeaga dunia Ijumaa ya tarehe 17 January,2014 katika hospitali ya Mount Ukombozi na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 19 January, 2014 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikishiriki misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika mwishoni mwa Juma jijni Dar.
Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai akimrithisha kiti alichopenda kukaa marehemu wakati wa ibada za Jumapili kanisani hapo mmoja wa watoto wa Mzee Arnold Nkhoma Bw. Amos Nkhoma.
Baadhi ya wajukuu na vitukuu wa Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma, wakiwa kwenye misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika jijini Dar.
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikitoka kanisani mara baada ya misa maalum.
Babu wakiwa na mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Nkhoma.
Michael Nkhoma, ndiyo mtoto mkubwa wa marehemu, akiongea na mdogo wake Amos Nkhoma. Kulia ni Aidan Nkhoma.
Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na baba yake mkubwa Michael Nkhoma,(kushoto) na Mzee Aidan Nkhoma.
Mama na Mwana wakijichukua taswira.
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma wakiwasha mishumaa kwenye kaburi la Mzee Arnold Nkhoma mara baada ya misa maalum ya shukrani iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mmoja wa vitukuu wa Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la babu yake.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.AMEN.
Ndugu, jamaa na marafiki walipojumuika nyumbani kwa nyumbani kwa Profesa Alice Nkhoma Wamunza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa ajili ya chakula cha mchana.
Profesa Alice Nkhoma Wamunza, akiongoza ndugu, jamaa na marafiki kwenye chakula mchana baada ya misa ya shukrani ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma.
Kwa picha zaidi ingia hapa
0 Comments