John Kerry akutana na Serguei Lavrov kuhusiana na taharuki kuhusu Ukraine
Waziri wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa baina yake na mwenzake kutoka Urusi Sergei Lavrov, katika mkutano wa dharurakuhusu mzozo wa Ukraine.
Marekani inasisitiza kuwa hatua ya urusi kutwaa eneo la Crimea baada ya kura ya maoni sihalali.
Bwana Lavrov ametoa masharti makali yasiyoegemea upande wowote huku akitaka uhuru wa Ukraine kama taifa utambuliwe.
Waziri wa Urusi amesema kuwa ni jukumu la Kiev kuandaa katiba mpya ili kuwezesha hilo lifanyike, mbali na kulinda maisha ya waukraine wachache wanaozungumza kirusi dhidi ya uvamizi kutoka kwa
waukraine wanaounga mkono kujiunga na jumuiya ya Ulaya.
Marekani imetaka hatua ya kuongeza wanajeshi zaidi wa Urusi katika mpaka mashariki ya Ukraine kukomeshwa mara moja.
Mazungumzo ya Paris siku ya ijumaa yalifuatwa na mazungumzo ya simu kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Obama wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Washington siku ya
Jumamosi, Bwana Kerry alibadilisha mkondo na kuelekea Paris.
Ukraine inasisitiza kuwa Urusi ina njama ya kuigawanya Ukraine na kulisambaratisha kama taifa.
Waandishi wanasema kuwa Maafisa wa Marekani wamegawanyika iwapo mazungumzo hayo yaliyopangwa yametokana na nia halisi ya Urusi ya kujaribu kupunguza taharuki iliyopo au ni mipango ya
hatua zaidi ya kijeshi.
Pentagon inaamini kuwa maelfu ya wanajeshi wa Urusi wamekita kambi karibu na mpaka na Ukraine kwa niya ya kuwatishia viongozi wa Ukraine .
|
0 Comments