Stori: Erick Evarist
MKALI wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ amefunguka kuwa wasanii wengi wa Kibongo hawaelewi maana ya bifu na faida zake.Baby alisema wasanii wanapaswa kuiga mifano ya wasanii wa nje, wanaotumia bifu kuongeza mkwanja na umaarufu pia.
“Hapa wanaendekeza majungu, wenzetu wakikosoana kimuziki, wanatengeneza kiki ya kibiashara na baadaye wanaitumia kuingiza chapaa, hawachukiani kutoka moyoni ila wanakosoana kiukweli,” alisema Baby.