Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh akiteta jambo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa toleo jipya la gari aina ya Mercedes Benz E-Class uliofanyika jijini Dar kwenye hoteli ya Capetown Fish Market.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw.Wayne McIntosh (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed (wa pili kushoto) wakibadilishana mawazo na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class uliofanyika kwenye hoteli ya Capetown Fish Market jijini Dar.(Picha na Zainul mzige)
.Ni E-Class inaweza kutembea bila dereva
.Pia inafaa kwa matumizi yoyote na imara
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
KAMPUNI ya CFAO Motors Tanzania hivi karibuni wamezindua gari mpya aina ya Mercedes-Benz E-Class Saloon na Estate yenye muonekano bora zaidi na inaweza kutembea bila dereva amesema Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo.
Akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es Salaam katika uzinduzi rasmi wa gari hilo la Meredes-Benz, E-Class, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania, Wayne McIntosh amesema gari hiyo nia aina mpya kabisa na kisasa zaidi kutengenezwa na kampuni hiyo.
“wakati wa majaribio nchini Ujerumani gari hii iliweza kutembea kilometa kadhaa bila kuwa na dereva kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu kabisa,” amesema McIntosh.
Wanenguaji wa kizungu wa Maendeleo Dance Group wakiburudisha tukio hilo la uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class jijini Dar es Salaam.
Amesema gari hiyo imetengezwa kwa ubunifu na teknolojia ya hali ya juu kabisa na wataalamu na mainjia kutoka nchini Ujerumani wenye uzoefu na utalaamu wa juu duniani.
McIntosh alisisitiza kwamba gari hiyo inaweza kabisa kutumiwa na mtu yoyote hapa duniani kutokana na muundo wake na teknolojia iliyotumika ni ya kisasa kabisa kumwezesha dereva au mtumiaji kuwa katika hali ya utulivu wakati wote wa safari.
“gari hii ni ya kimataifa yenye uwezo wa kumudu aina yeyote ya misukosuko barabarani na ni salama kwa mtumiaji wakati wote,” aliongeza.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania, Wayne McIntosh akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa gari hiyo mpya katika soko la Tanzania kwenye hoteli ya Cape Town Fish Market Msasani jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh, akizindua rasmi Mercedez Benz aina ya E-Class jijini Dar esSalaam kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye hoteli ya Capetown Fish Market.
Sasa imezinduliwa rasmi katika soko la Tanzania.
Toleo jipya la gari aina ya Mercedes Benz E-Class lililozinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam na kampuni ya CFAO Motors.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia tukio hilo la kipekee.
Mmoja wa wageni waalikwa akionekana kuvutiwa na toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Mwakilishi wa TV 1 kutoka nchini Ghana akipozi na gari matata aina ya Mercedes Benz E-Class kwenye hafla fupi ya uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Muonekano wa ndani wa gari hilo lenye speed 260.
Mmoja wa models aliyepamba uzinduzi huo akipozi kwenye toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Muonekano wa nyuma.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania, Bi.Margareth Chacha akifanyiwa mahojiano na TV1 ambapo akielezea mapenzi yake na magari ya aina ya Mercedes Benz ambapo hapo awali alikuwa akitumia na panapomajaliwa ya Mungu siku moja atamiliki toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Tharaia Ahmed akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania, Bi.Margareth Chacha kwenye hafla hiyo. Katikati ni Hellen Kiwia kutoka Frontline Management.
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifafanua jambo kwa mmoja wa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Wayne McIntosh, akisalimiana na mmoja wa wageni waalikwa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake Tanzania, Bi.Margareth Chacha (kushoto) kwenye hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa toleo jipya la Mercedes Benz E-Class. Katikati ni Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi.
Crew ya stesheni mpya ya TV 1 nao waliokuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.
0 Comments