Stori: Imelda Mtema
STAA wa Number One Remix, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema vipo vitu vingi anavyovipenda kwa mpenzi wake, Wema Sepetu lakini suala la mapishi ndilo linachukua nafasi kubwa.“Wema nampenda kwa mengi ujue lakini pia anajua sana kupika mapochopocho ndiyo maana sipindui, mwanamke mapishi bwana,” alisema mwanamuziki Diamond.