Maafisa wa polisi wakikagua eneo kulikotokea mlipuko siku zilizopita jijini Nairobi. |
Picha za televisheni zinaonyesha mabasi hayo yakiwa yameharibiwa na madirisha kuvunjika.Ni hapo jana tu ambapo watu wanne waliuawa na wengine wapatao ishirini kujeruhiwa katika shambulio lingine ambapo grunedi ilirushwa katika kituo cha mabasi ya abiria. Shambulio la pili lilitokea karibu na mkahawa mmoja maarufu lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa.Mashambulio haya yanatokea mwezi mmoja tu baada ya serikali kuanzisha oparesheni ya usalama baada ya kukumbwa na mashambulio mengine hapo awali na pia kupata vitisho kutoka kwa kundi la wanamgambo wa Alshabab waliodai kutekeleza shambulio la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.
0 Comments