Katika kutambua umuhimu na upendo kwa wenzetu wa nyumbani Tanzania wanaopata shida katika huduma za  matibabu na mambo muhimu ya kibinaadamu,Kikundi kidogo cha Upendo Women's Group kilichopo Brussels nchini Ubelgiji kimeandaa chakula cha pamoja cha jioni kwa wageni waalikwa ambao watahudhuria sherehe kwa siku hiyo.

Lengo ni kuchangishana kwa kile tulichoaajaliwa ili kuwasaidia ndugu zetu wanaopata shida katika mambo muhimu ya msingi katika jamii..

Balozi Kamala atakuwepo.
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh:Kamala ni mmoja wa wageni waalikwa siku hiyo,kwa hivyo ni fursa yako ndugu mtanzania kukutana na Balozi wako kwenye tafrija hiyo.

Ngoma za Asilia na Taarabu
Kutakuwa na ngoma za kiasili na Taarabu kwa siku hiyo hapo ukumbini.

Chakula 
Kutakuwa na Buffet na kila mmoja aamini kwamba atafurahia chakula siku hiyo.

Muziki
Patachezwa muziki kwa kila mwenye kupenda muziki

Muda
Shughuli zitaanza saa kumi kamili jioni16:00 na kuisha saa tano za usiku 23:00.
Itapendeza kama ukija na wenzako wengi ili kuonyesha upendo kwa wanaupendo wa umoja huo.

Ukiliona tangazo hili hautapata dhambi ukimwambia na mwenzako.
Watu wote mnakaribishwa.