|
Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Mamia ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba zikihofia usalama wao.
|
Gazeti la The Telegraph linasema kuwa takriban watalii 500 kutoka Uingereza wataathirika na kauli hiyo.
Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya.
Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.
Watalii kutoka Uingereza watoroka mashambulizi pwani ya Kenya
Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa.
Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.
0 Comments