Wachezaji sinema, Daniel Day-Lewis na Angelina Jolie, wametukuzwa na Malkia Elizabeth wa Uingereza katika orodha anayotoa kila mwaka kuwatunza watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii.
Daniel Day-Lewis atapewa cheo cha Sir, na Angelina Jolie atapewa cheo cha Dame kwa kampeni yake ya kupambana na uhalifu wa ubakaji wa wanawake katika maeneo ya vita, pamoja na kazi zake nyengine kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR.Na waandishi wawili wa BBC wamepata nishani ya OBE:
Lyse Doucet, mwandishi mkuu wa BBC katika maswala ya kimataifa, na Tin Htar Swe, mhariri wa Idhaa ya BBC ya lugha ya Burma.
Stephen Sutton, kijana wa miaka 19 aliyekufa karibuni kutokana na saratani, na wakati akiugua aliongoza mchango wa karibu dola milioni 7 kugharimia utafiti dhidi ya ugonjwa huo, ametunzwa MBE, (ambayo alipokea kabla ya kufariki mwezi uliopita.)
Mtunzi wa riwaya, Hilary Mantel, aliyeandika vitabu vilivyopata zawadi ya Booker, 'Wolf Hall' na 'Bring up the Bodies', piya amepewa hadhi ya Dame.
|
0 Comments