uhusiano wa Somalia na Marekani
Rais Barack Obama anatarajiwa kumteua balozi wa kwanza wa wa Somalia, mara ya kwanza tangu nchi hiyo itumbukie katika vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Waziri msaidizi wa masuala ya siasa nchini Marekani, Wendy Sherman amesema kuwa hatua hiyo inaashiria imani ya Marekani kwa Somalia na kuwa ni ishara ya uhusiano mwema kati ya nchi hizo mbili.
Japo Marekani haikuwahi kuvunja rasmi uhusiano na Somalia ililazimika kufunga ubalozi wake mwaka wa 1991 baada ya vita kuanza.
Miaka miwili baadaye, wanajeshi 18 wa Marekani waliuawa katika makabiliano na wapiganaji wa kikoo nchini Somalia jambo lililosabaisha Marekni kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini humo.